Kwa mujibu wa Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Bw. Suhail Chaudhry, Imam wa Ijumaa na wa Swala za Jamaa wa Msikiti wa Lansing Mashariki, alisema: Waislamu katika eneo hili wamekuwa wakikumbana moja kwa moja na kwa namna inayoonekana wazi na hali ya chuki dhidi ya Uislamu.
Chaudhry aliongeza: “Kundi la watu linatoa kauli za kupinga na kumtukana Mtume wetu Mtukufu Muhammad (saww). Hivi karibuni tatizo hili pia limehamia katika anga ya mtandao, Kwa masikitiko baadhi ya watumiaji huko magharibi mwa Michigan wamekuwa wakiwataja Waislamu kuwa ni ‘saratani’ na ‘waovu.’”
Akieleza kwamba kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu ni jambo muhimu kwa makundi yote, aliongeza: “Kila mmoja anapaswa kukusanyika na kusimama dhidi ya ubaguzi huu na uchochezi wa chuki; kwa sababu tusipofanya hivyo, hali hii itazidi kuwa mbaya na sote tutaathiriwa na moto wake.”
Chaudhry alibainisha kwamba; milango ya “Msikiti wa Lansing Mashariki” iko wazi kwa kila mtu anayependa kufanya mazungumzo au kupata taarifa zaidi kuhusu Waislamu.
Bi. Nazita Lajvardi, profesa wa Chuo Kikuu cha Michigan anayefanya utafiti kuhusu chuki dhidi ya Uislamu na chuki dhidi ya Wayahudi, alisema kwamba; matukio haya ni sehemu ya mwenendo mpana zaidi. Lajvardi alisema: “Kundi hili la watu kwa hakika linakabiliwa na kiwango kikubwa zaidi cha ubaguzi na uhalifu unaochochewa na chuki.”
Lajvardi aliongeza: Ubaguzi dhidi ya jamii za Waislamu umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni, na mambo mbalimbali, yakiwemo migogoro inayoendelea katika Mashariki ya Kati, yana mchango katika hali hiyo.
Chanzo: wilx.com
Maoni yako